MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAHUSISHA KATIKA BIASHARA.

Kama mfanyabiashara, kuna wakati unatamani biashara yako ipate kujulikana na kuwafikia walengwa wengi zaidi. Pia kuna wakati utakumbana na changamoto nyingi sana katika uendeshaji wa biashara yako na hata kukufanya uchoke na kuhisi kukata tamaa.

Leo tunaenda kuzungumzia mambo muhimu matano(5) yatakayokusaidia katika kufanya biashara yako ikue na kupata kujulikana kwa walengwa(wateja wako). Pia namna ya kuepuka au kupunguza changamoto za uendeshaji wa biashara yako kadri inavyozidi kukua.

mambo muhimu matano(5) yatakayokusaidia katika kufanya biashara yako ikue na kupata kujulikana kwa walengwa(wateja wako)

Mambo matano(5) muhimu unayopaswa kuyahusisha katika biashara
1. Mitandao ya kijamii

2. Mifumo ya Kidigital

3. Vyombo vya Habari

4. Vipeperushi

5. Maonyesho ya kibiashara

Mitandao ya kijamii. Moja ya sehemu ambayo inakuwezesha kukuza jina la biashara yako na pia kuwafikia wateja wengi zaidi ni katika mitandao ya kijamii. Ukichunguza kwa makini utagundua kua kila biashara yenye kufanikiwa vizuri inajihusisha na kujitangaza vyema sana kwenye mitandao ya kijamiii. Wewe unachopaswa kufanya ni kufungua page ya biashara katika mtandao wowote wa kijamii, na kisha kuanza kupost(kuweka) matangazo ya bidhaa zako.

Baadhi ya mitandao ya kijamii iliyo maarufu zaidi.
· Facebook

· Instagram

· Twitter

· LinkedIn

· Redit n.k

Mifumo ya Kidigital. Kadiri biashara yako inavyokua, ugumu katika uendeshaji nao huongezeka, namaanisha... (Changamto katika utunzaji wa kumbukumbu za mapato, manunuzi na matumizi) huongezeka. Pia namna rahisi ya kuwahudumia wateja inakua changamoto pindi wanapozidi kuongezeka. Sasa haipaswi kua hivyo, Lengo ni kukuza biashara na kuifanya ipate wateja wengi zaidi. Ili kuhakikisha unaweza kuendana na spidi ya ukuaji wa biashara yako, ni muhimu sana kuhusisha matumizi ya teknolojia ya mifumo katika kukusaidia usimamizi au uendeshaji wa biashara yako.

Baadhi ya mifumo ambayo unaweza itumia katika biashara yako.
· SkyMicrofinance. Kwaajili ya uendeshaji wa shughuli za utoaji mikopo. Fahamu zaidi kuhusu SkyMicrofinance

· SkyStock. Unasaidia katika usimamizi au uendeshaji wa biashara kwa kuratibu shughuli zote za manunuzi, mauzo na matumizi na utunzaji wa kumbukumbu kwa wafanyabiashara wakubwa. Fuatilia zaidi kuhusu SkyStock

· SkyMkoba. Unatumika kuhifadhi kumbukukumbu za mapato na matumizi kwa wafanyabiadhara wadogo na wakati. Fahamu zaidi kuhusu SkyMkoba

· SkyGulio. Unakuwezesha kufanya mauzo ya biadhaa zako za gengeni. Kama mbogamboga, matunda n.k Fahamu zaidi kuhusu SkyGulio

Vyombo vya habari. Endapo kama ni mfanyabiashara mwenye uwezo kifedha, si vibaya pia kuhusisha utumiaji wa vyumbo vya habari kama vile, Televisheni, Redio na Magazeti katika kuitangaza biashara yako au kuwafikia wateja wengi zaidi. Naamini wengi tumekwisha ona biashara nyingi kubwa tuu na hata zile zilizotoka kuanzishwa zikitangazwa kwenye televisheni au maredioni.

Vipeperushi. Wakat mwingine unaweza kutumia vipeperushi kama njia ya kuitangaza biashara yako. Pindi mteja anapokuja unaweza muachia kipeperushi apate kusoma na kufahamu zaidi kuhusus biashara yako (bidhaa na hata huduma nyinginezo unazotoa). Wakati mwingine vipeperushi hivi huweza kutumika kwenye maonyesho au semina mbali mbali za kibiashara.

Maonyesho ya kibiashara. ni muhimu sana kuhudhuria maonyesho mbalimbali ya kibiashara kama vile, SabaSaba , Nane Nane, n.k. Hii ni njia mojawapo ya kuitambulisha biashara yako kwa wateja na kufanya bidhaa zako zipate kufahamika zaidi. Kumbuka, kadiri bidhaa zako au huduma zako zinavyozidi kufahamika ndivyo wateja wanavyozidi kuongezeka na biashara yako kukua.