NAMNA YA KUONGEZA THAMANI KATIKA BIASHARA

Kukua kwa biashara kunategemea na namna mtu anavyojitahidi katika kuifanya biashara yake iwe na thamani zaidi. Thamani mbele ya wateja na pia thamani kwa wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza katika biashara yake.

Biashara ni nini ?

“Biashara ni shughuli au mchakato wa kununua na kuuza mali au vitu. Inaweza kufanywa na mtu binafsi au kwa ushirikiano au na jamii au nchi kwa jumla”. wikipedia

Ongeza thamani katika biashara yako

FAIDA 3 ZA KUONGEZA THAMANI YA BIASHARA

Faida zinazoweza kutokana na kuongezeka kwa thamani ya biashara yako ni pamoja na:-

1. Kupata urahisi katika kuomba mikopo. Unapoomba mkopo, kampuni husika au benki hufanya uthaminishaji wa biashara yako na kuona imebeba thamani kiasi gani, ili kuwa na imani ya kutoa mkopo.

2. Kuvutia wateja wengi zaidi. Wateja hupendelea kununua bidhaa kwa mtu mwenye kuonyesha kuithamini biashara yake, wakiamini kuwa atakuwa ni mtu mwenye kuwathamini wateja wake pia. kwa maana thamani ya biasha hujengwa pia kwa namna mtu anavyowathamini wateja wake.

3. Kuvutia wawekezaji. Ni rahisi sana kumpata mtu atakayewekeza katika biashara yako ikiwa kama sehemu ya kupata mtaji na kuikuza endapo utakuwa mwenye kuonyesha kuithamini biashara katika hali ya awali ya udogo ilionao.

Njia Tano zinazoweza kuongeza thamani katika biashara yako

NJIA 5 ZINAZOWEZA KUONGEZA THAMANI YA BIASHARA

1. Kuendana na ukuaji wa teknolojia. Kutumia teknolojia katika biashara, kunasaidia kuongeza ufanisi na kurahisisha mawasiliano kati yako na wateja. Hii hufanya biashara yako kuonekana yenye kukua na kuendana na wakati (zama za teknolojia).

2. Utayari wa kutumia mifumo. Biashara yenye kukua ni ile yenye kusimamiwa kwa ustadi na umakini bila kutumia nguvu nyingi. Mifumo hukurahisishia katika kusimamia biashara yako katika mauzo, manunuzi, matumizi, stock zilizopo stoo na hata mishahara ya wafanyakazi pia kujua faida au hasara ya biashara na chanzo cha hasara, hivyo unajua muelekeo wa biashara yako. Ipo mifumo mingi, Mfumo wa SkyStock, ni moja kati ya mifumo bora zaidi.

sasa unaweza kuendesha biashara yako kidigitali

3. Wajue wateja wako; jua kipato chao ili uweze kuuza bidhaa wanazoweza kumudu bei yake, fahamu zaidi bidhaa wanazozipenda ili kuongeza mauzo, waonyeshe kuwathamini wakati unapowahudumia kwa kuwapa huduma kwa wakati na kusikiliza mapendekezo yao.

4. Matangazo yanayolenga wateja na biashara yako. Kutangaza bidhaa au biashara yako ni jambo kubwa na la muhimu sana, ili kuongeza idadi ya wateja na hata kufahamika kwa biashara yako. Kukosea kuandaa matangazo yenye tija na rahisi kuiwasilisha biashara yako kwa wateja huweza kuwa chanzo cha upotevu wa fedha na kuporomoka kwa biashara.

5. Jikite kwenye kutoa huduma/bidhaa bora na sio bora huduma/bidhaa. Bidhaa bora huongeza mvuto na ushawishi kwa watumiaji. Hivyo ni rahisi kuongeza wateja wengi na kuongeza uthamani katika biashara yako.

UFUPISHO KWA NJIA YA PICHA

faida  za kuongeza thamani ya biashara yako