UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU KWA MFUGAJI
Kumbukumbu au kuweka record katika ufugaji ni muhimu sana, wafugaji wengi wanajisahau kufanya hivyo, mwisho wa siku wanajikuta hawajui faida ni ipi, pia wanashindwa kujua wamepata hasara kwa ukubwa gani, kumbukumbu ni muhimu sana ndio maana kuna msemo unasema "MALI BILA DAFTARI HUISHA BILA HABARI."
Wabunifu wa Kitanzania wamefanikiwa kubuni mfumo kwa ajili ya kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu za kifedha katika kusimamia miradi yako ya ufugaji, Mfumo huu unajulikana kwa jina la SkyMkoba, mfumo wa SkyMkoba utakusaidia.
-
Kusimamia mradi kwa ufanisi
-
Kujua uwiano wa mapato na matumizi
-
Kukuonyesha faida na hasara kwenye mradi
-
Kuwa na taarifa sahihi za mradi kwa ajili ya kurahisisha uombaji wa mikopo ya kukuza mradi
-
Kuongeza uaminifu baina ya wabia wa mradi
-
Kuwa na usalama wa taarifa pamoja na urahisi katika upatikanaji
Namna ya kutumia mfumo wa SkyMkoba katika miradi ya ufugaji
Ufugaji wa Ng’ombe
Katika kuhakikisha unasimamia vyema mradi wako, taarifa zote zinazohusu matumizi ya fedha pamoja mapato zinatakiwa kutunzwa, mfano wa taarifa za kutunza kweye App ya SkyMkoba ni:-
-
Gharama za marisho na maji
-
Gharama za dawa, chanjo na kinga za magonjwa
-
Malipo ya wafanyakazi/wasimamizi
-
Mauzo ya maziwa
-
Mauzo ya ng’ombe waliofikia umri wa kuuza nk
Ufugaji Nyuki
Epukana na hali ya kutokufahamu kiasi cha fedha unachotumia katika kusimamia mradi na kiasi kinachoingia baada ya kufanya uzalishaji wa zao la nyuki, Ni muhimu taarifa kutunza kumbukumbu ya fedha, mfano kumbukumbu zifuatazo
-
Gharama za kutengeneza mizinga
-
Gharama za kununua mashine ya kukamulia
-
Gharama za mavazi
-
Mauzo ya asali
-
mauzo ya NTA (BEESWAX)
-
Mauzo ya CHAVUA (POLLEN)
Ufugaji wa Samaki
Uhitaji ya wa samaki katika jamii zetu ni mkubwa sana, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na uzalishaji mkubwa wa samaki kupitia ufugaji wa kwenye mabwawa, ili kuhakikisha unafanya uzalishaji mkubwa ni vizuri kuwa na usimamizi mzuri wa mradi katika upande wa mapato na matumizi ya fedha. Ni muhimu kutunza kumbukumbu zote, mfano
-
Gharama za ujenzi wa bwawa
-
Manunuzi ya chakula
-
Malipo ya wasimamizi wa mradi
-
Gharama za kinga ya magonjwa
-
Mauzo ya Samaki
Ufugaji wa nguruwe
Jambo muhimu katika kusimamia vizuri mradi wa nguruwe ni kuhakikisha kuwa taarifa zote za kifedha zinatunzwa vizuri na zinafahamika, hivyo ni vyema kutumia njia ya kisasa ya kutunza kumbukumbu hizo, kwa sasa unaweza kutumia aplikesheni ya SkyMkoba, mfano wa taarifa ambazo unaweza kutunza:
-
Ununuzi wa nguruwe watoto
-
Ujenzi wa banda
-
Gharama za Chakula
-
Gharama za Dawa na kinga
-
Mauzo ya nguruwe waliofikia umri wa kuuzwa.
Ufugaji wa kuku
Ufugaji wa kuku wa nyama pamoja na mayai umeendelea kuwa muhimu sana hasa kwa kuku wa kienyeji, hii ni kutoka na kuwa jamii nyingi zinapendelea sana ulaji wa kitoweo cha kuku pamoja na mayai, ni vyema zaidi kutumia njia za kisasa katika kusimamia mradi ili uweze kuwa na uzalishaji mzuri na mkubwa, utunzaji wa kumbukumbu za fedha zinatumika na kupatikana kwenye mradi ni muhimu, hivyo tumia njia ya kisasa ya Aplikesheni ya SkyMkoba, mfano wa taarifa ambazo unaweza kuhifadhi kwenye Aplikesheni ya SkyMkoba ni:-
-
Gharama za kununua vifaranga
-
Gharama za dawa, chanjo na kinga
-
Gharama za chakula
-
Mauzo ya kuku
-
Mauzo ya mayai
JINSI YA KUJIUNGA NA MFUMO WA SkyMkoba
Tafuta neno SkyMkoba kuipakua Aplikesheni hii kwenye Play Store au bofya linki hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.a2daysky.wallet, kama unatumia compyuta bofya link hii https://skymkoba.com
Kupata msaada zaidi wasiliana na watoa huduma wetu kwa simu: 0693 157 655.