UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU KWA MKULIMA
Utunzaji wa kumbukumbu katika jamii za wakulima umeendelea kuwa changamoto kubwa ambayo inayorudisha nyuma maendeleo katika kilimo faida, Asilimia kubwa ya wajasiriamali katika kilimo bado hawana tabia ya kutunza taarifa za gharama wanazotumia katika uzalishaji pamoja na mapato wanayoyapata baada ya kuuza mazao yao.
Hii ni kutokana na kuwa, njia zilizopo si rahisi na salama kwao kuzitumia kutokana na mazingira ya kazi hiyo, mfano kutumia notebook ambapo ni vigumu kutembea na notebook kila wakati, na matumizi ya excel si rafiki kwa mkulima.
Kwa kutambua ukubwa wa changamoto hii, tumefanikiwa kupata suluhu kwa kuwa na Aplikesheni rahisi na ambayo haitumii internet kwa ajili ya kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu za kifedha kwa wakulima. App hii inajulikana kwa jina la SkyMkoba. Kwa sababu muda mwingi mtu unakuwa na simu yako, itakuwa rahisi sana kwako kutunza taarifa kwenye App ya SkyMkoba.
Umuhimu wa kutunza taarifa za usimamizi wa kilimo kwenye App ya SkyMkoba
-
Kufahamu kwa urahisi faida unayoipata katika kilimo chako
-
Kujua gharama zote za uzalishaji ili kuweza kupanga bajeti ya msimu mwingine unaokuja.
-
Kupata taarifa sahihi za uendeshaji wa kilimo, taarifa hizi unaweza kuzitumia katika kuomba mikopo kwenye taasisi za kifedha
-
Kuwa na uhakika wa upatikanaji na usalama wa taarifa, taarifa zote zitafanyiwa automatic backup, hivyo itakuwa rahisi kuzipata pale zinapohitajika,
-
Kuongeza uaminifu baina ya wanakikundi au wanafamilia, kwani taarifa zote za matumizi ya fedha katika uzalishaji,uvunaji, na fedha za mapato baada ya kuuza mazao zitakuwepo kwenye App.
-
Kuondokana na upotevu wa taarifa kama unatumia notebook
NAMNA YA KUTUMIA SkyMkoba KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA KILIMO
KILIMO CHA MBOGAMBOGA
Ni muhimu ewe mkulima kujiwekea kumbukumbu za uzalishaji, mapato na faida katika kilimo chako cha mbogamboga ili kuweza kupima mafanikio ya kazi unayoifanya.
Mfano wa taarifa ambazo unaweza kuweka kwenye App ya SkyMkoba
-
Gharama za kununua mbegu
-
Gharama za kununua mbolea
-
Manunuzi ya dawa za kuua wadudu
-
Manunuzi ya vifaa vya kilimo
-
Gharama za kuvuna na kusafirisha kwenda sokoni
-
Mapato yaliopatikana baada ya kuuza
KILIMO CHA MATUNDA
Uhitaji wa matunda katika afya ya binadamu ni muhimu sana, hivyo mahitaji na upatikanaji wa matunda ya aina mbalimbali ni mkubwa, ili kuhakikisha unakuwa na uzalishaji pamoja na usimamizi mzuri, ni vizuri kutunza taarifa za mapato na matumizi ya fedha katika kilimo chako kidigitali ukiwa na App ya SkyMkoba. Mfano wa taarifa ambazo unaweza kutunza kwenye SkyMkoba.
-
Gharama za kununua miche
-
Manunuzi ya mbolea
-
Dawa ya kuua wadudu
-
Taarifa za mauzo ya matunda (maembe, machungwa, nanasi, matango nk)
-
Gharama za vifaa vya umwagiliaji
-
Gharama za maji (gharama za kuchimba kisima)
KILIMO CHA MAHINDI
Ili kuhakikisha unaenda na wakati na kufanya kilimo cha kisasa, ni muhimu pia kuwa na tabia ya kutunza kumbukumbu ya fedha zinazotumika katika uzalishaji pamoja na zile zinazopatikana baada ya kuuza, hiki kinawezekana unapokuwa na App ya SkyMkoba ambayo ni daftari la kidigitali unalokuwa nalo wakati wote kwenye simu janja yako.
Mfano wa Taarifa ambazo unaweza kutunza kwenye App ya SkyMkoba:-
-
Gharama za kuandaa shamba
-
Manunuzi ya mbolea
-
Manunuzi ya mbegu bora
-
Gharama za kulima, (kulipia trekta litakalolima shamba)
-
Manunuzi ya dawa za kuulia wadudu
-
Gharama za kufanya palizi
-
Gharama za kuvuna na kusafirisha kupeleka sokoni
-
Mapato baada ya kuuza mahindi
JINSI YA KUJIUNGA NA MFUMO WA SkyMkoba
Tafuta neno SkyMkoba kuipakua Aplikesheni hii kwenye Play Store au bofya linki hii https://play.google.com/store/apps/details?id=com.a2daysky.wallet, kama unatumia compyuta bofya link hii https://skymkoba.com
Kupata msaada zaidi wasiliana na watoa huduma wetu kwa simu: 0693 157 655.