NAMNA TEKNOLOJIA INAVYOWEZA KUKUZA BIASHARA YAKO

Utangulizi

Katika ulimwengu huu wa teknolojia, mambo mengi sana yamepata kurahisishwa na hata kupelekea uongezekaji wa ufanisi katika utendaji kazi na hata kuchangia katika kuboreshwa kwa mawasiliano na mengine mengi.

Sekta ya biashara ni miongoni mwa maeneo ambayo yamepata kukua kwa kasi zaidi. Katika zama hizi za teknolojia, biashara nyingi zimekuwa zikifanyika mtandaoni(internet), na kurahisisha ulipaji na uwasilishaji wa bidhaa au huduma kwa wakati. Hii yote ni kutokana na ukuaji wa teknolojia.

Teknolojia ni nini ? “Teknolojia ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.” Wikipedia

MATUMIZI 7 YA TEKNOLOJIA KATIKA KUKUZA BIASHARA YAKO

1. Matangazo

2. Mauzo na manunuzi

3. Kukusanya wateja

4. Ushirikiano na kujifunza

5. Kuongeza ufanisi

6. Huduma kwa wateja

7. Urahisi katika utafutaji na uagizaji wa bidhaa mpya.

Matangazo. Teknolojia inakuwezesha kutengeneza matangazo ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza biashara yako mfano video na vipeperushi .Pia kwa kutumia teknolojia ni rahisi sana kuitangaza biashara yako katika mitandao ya kijamii, kwenye televisheni au hata radio na magazeti.

Mauzo na manunuzi. Unaweza kutumia teknolojia katika kuratibu au kusimamia mauzo na manunuzi yote katika biashara yako. Hii ni kwa kutumia mifumo maalum iliyoundwa kwa kazi hiyo. Mafano mifumo kama SkyStock na SkyMkoba, hii ni moja kati ya mifumo itakayokuwezesha kufanya yote hayo, pia hata kukusaidia katika utunzaji wa kumbukumbu zote za kibiashara.

Kukusanya wateja. Kwa kupitia barua pepe ni rahisi zaidi kuwaweka wateja wako karibu zaidi na biashara yako. Pia unaweza kutumia mitandao ya kijamii, kukusanya wateja wako sehemu moja na kuwaweka karibu zaidi.. kwa kutengeneza makundi au kurasa zinazohusiana na huduma au bidhaa zako. Kufanya hivi kutakusaidia kuwa na wateja au wafuatiliaji wa kudumu wa bidhaa au huduma zako.

Ushirikiano na kujifunza. Kwa kutumia teknolojia ni rahisi kushirikiana na wafanyabiashara wengine au wawekezaji, katika kuhakikisha masuala ya kibiashara na mipango mbalimbali inakwenda sawa. Mfano, kufanya vikao mbalimbali vya kibiashara kwa njia ya video au sauti, kutoa mafunzo mbalimbali kwa njia ya mtandao kwa wateja au wafanyakazi wako. Pia hukurahisishia katika kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na biashara yako katika mitandao na kujiongezea maarifa zaidi.

Kuongeza ufanisi. Unaweza kutumia teknolojia kuongeza ufanisi wa biashara yako, mfano utunzaji wa kumbukumbu za mauzo na manunuzi, katika kuwasiliana na wateja wako, Kufanya mauzo na manunuzi, kupokea order(oda) mbalimbali na kufanya delivery(uwasilishaji).

Huduma kwa wateja. Unaweza kutumia teknolojia kurahisisha suala la huduma kwa wateja. Mfano unaweza tumia teknolojia kuboresha mawasiliano na wateja, kuboresha namna ya kuchangamana na wateja(Mfano. kwa kutumia aplikesheni au maroboti(online customer care agents)) katika kujibu maswali ya changamoto mbalimbali wateja wanazokumbana nazo, au katika kuwapatia maelekezo mbalimbali.

Urahisi katika utafutaji na uagizaji wa bidhaa mpya. unaweza kununua kitu hata nje ya nchi kwa kukiona kwenye mitandao ya kijamii, au tovuti za kibiashara mfano. Ebay, Amazon, AliExpress n.k na ukafanya malipo yote mtandaoni na ukatumiwa hadi ulipo ndani ya muda mfupi.

matumizi 7 ya teknolojia katika kukuza biashara